🏆 REKODI 10 ZA KOMBE LA DUNIA ZIONEKANAZO HAZITAVUNJWA MILELE
Wakati Staa kama Lionel Messi, Cristiano Ronaldo na Kylian Mbappé wakitarajiwa kuandika historia mpya katika Kombe la Dunia 2026, bado zipo rekodi ambazo zinaonekana kuwa ngumu sana kuvunjwa.
Baadhi ya rekodi hizi zinazoweza kudumu milele katika vitabu vya historia ya soka ni:
🥇 1. Pele kutwaa Kombe la Dunia mara tatu
Gwiji huyo wa Brazil ndiye mchezaji pekee aliyewahi kushinda Kombe la Dunia mara tatu (1958, 1962 na 1970).
⚽ 2. Just Fontaine kufunga mabao 13 katika Kombe moja
Mfaransa huyo aliweka rekodi hiyo mwaka 1958, rekodi iliyodumu kwa karibu miaka 70.
😲 3. Kufunga mabao manne na bado ukafungwa
Ernst Wilimowski wa Poland alifunga mabao manne dhidi ya Brazil mwaka 1938, lakini timu yake ikapoteza 6-5.
👴 4. Roger Milla kuwa mfungaji mkongwe zaidi
Alifunga akiwa na miaka 42 na siku 39 mwaka 1994.
🧤 5. Essam El-Hadary kuwa mchezaji mkongwe zaidi kucheza
Kipa wa Misri alicheza Kombe la Dunia 2018 akiwa na miaka 45.
🌍 6. Kuchezea mataifa matatu tofauti
Dejan Stanković aliwakilisha Yugoslavia, Serbia & Montenegro, na Serbia katika Kombe la Dunia.
🏅 7. Kufika fainali na mataifa mawili tofauti
Luis Monti alicheza fainali akiwa na Argentina (1930) na baadaye kutwaa ubingwa akiwa na Italia (1934).
👔 8. Kushiriki Kombe la Dunia mara sita kama kocha
Carlos Alberto Parreira ndiye kinara wa rekodi hiyo.
🟨 9. Mchezaji kupewa kadi tatu za njano katika mechi moja
Josip Šimunić alipokea kadi tatu za njano mwaka 2006 kutokana na kosa la mwamuzi Graham Poll.
👥 10. Mashabiki wachache zaidi kuhudhuria mechi🤓🤏
Takribani watu 300 pekee walishuhudia mechi ya Romania dhidi ya Peru katika Kombe la Dunia la 1930.
📖⚽ Baadhi ya rekodi huvunjwa, lakini nyingine huonekana kuandikwa milele katika historia ya mchezo.
#WorldCup2026
#Follow
Comments
Post a Comment